Msako wa mashoga nchini ethiopia

 

Mamlaka za Ethiopia zimesema zimekuwa zikikabiliana na hoteli, baa na maeneo ya burudani katika mji mkuu ambapo inadai vitendo vya ngono vya wapenzi wa jinsia moja vinafanyika.


Ofisi ya Utawala wa Amani na Usalama ya Addis Ababa, chombo cha serikali, ilisema ilikuwa ikichukua hatua "dhidi ya taasisi ambazo vitendo vya mapenzi ya jinsia moja vinatekelezwa".


Katika taarifa yake kwenye mtandao wa Facebook, mamlaka ya jiji hilo ilisema hatua hiyo ilikuja baada ya taarifa kutoka kwa umma, na kusema kuwa tayari ilikuwa imevamia nyumba ya wageni.


Imewataka wananchi kutoa taarifa kwa polisi kuhusu vitendo hivyo na kuongeza kuwa itaendelea na msako katika maeneo mengine.


Mapenzi ya jinsia moja ni marufuku nchini Ethiopia, lakini hakujawa na ripoti zozote za hivi majuzi za kesi au hatia zinazohusiana na vitendo hivyo.


Mapema wiki hii, kikundi cha utetezi cha LGBT, House of Guramayle, kilisema Ethiopia ilikuwa ikishuhudia "mashambulio ambayo hayajawahi kushuhudiwa kwa watu binafsi kulingana na mwelekeo wao wa kijinsia halisi au unaofikiriwa na utambulisho wa kijinsia".


Ilitoa wito kwa mashirika ya kutetea haki za binadamu mashinani na kwingineko kulaani mashambulizi kama hayo, na kuhimiza majukwaa ya mitandao ya kijamii kushughulikia video za matamshi ya chuki zinazoitishia vurugu.


Swali

Ni nchi gani ambazo mapenzi ya jinsia moja ni kinyume cha sheria? Je zina agenda gani?

Msomi wetu

Tembelea bloggers yetu kwa ajili ya kupata habari mbalimbali za michezo burudani elimu nakadhalika

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post